NYOTA wa muziki wa Bongo fleva, Saidi Juma ‘Chege Chigunda’ na
Snura Mushi, anayebamba na wimbo wa ‘Majanga’, wanatarajiwa kupamba shoo
ya Miss Mwanza itakayofanyika Juni 14.
Chegge na Snura, tayari wameshasainishwa mkataba wa kufanya shoo
kwenye shindano hilo kwenye Ukumbi wa Yacht Club, Capri Point,
Nyamagana, jijini hapa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, John
Dotto, inayoratibu shindano hilo, alisema maandalizi yanakwenda vizuri
kwani warembo wote 18 wanazidi kujifua.
“Tunajivunia aina ya warembo ambao tunao. Tumejitosheleza sana katika
eneo la ubora wa warembo, tunaamini Miss Mwanza mwaka huu ndiye
atashinda Miss Kanda ya Ziwa na baadaye Miss Tanzania,” alisema.
Mbali ya wadhamini wakuu Redd’s Premium Cold, Dotto aliwataja wengine
ni Global Publishers Ltd, Techno Mobile Phones, CXC Africa Ltd, Tanapa,
Liver Gold Mining, NIC Bank, Star TV, Mama Nyimbo Decoration, Clara
Salon na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

No comments:
Post a Comment