MODO mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Jacqueline Patrick (pichani) amefunguka kuwa baada ya kutemana na aliyekuwa mume wake, Abdullatif Fundikira hafikirii kuzaa miaka ya hivi karibuni.
Akichonga
na paparazi wetu juzikati jijini Dar, Jack alisema kwa sasa yeye na
kuzaa mbalimbali kwa vile ana mipango mingi ya maisha ingawaje anapenda
sana watoto.
“Napenda sana watoto lakini sitarajii kabisa kuzaa kesho
wala keshokutwa, kwasababu ni lazima ujipange sawasawa ili uweze
kumtunza vyema mtoto pindi utakapojifungua,” alisema na kuongea:
“Wanawake
wengi wanaharakisha kuzaa matokeo yake ni kuwaacha watoto nyumbani na
mahausigeli wakiwa wadogo ili wao wakatafute chochote, lazima ukae na
mwanao hata mwaka mmoja aweze kupata malezi bora ndiyo maana nasema
lazima ujipange sana.”
Credit:GLP
No comments:
Post a Comment