SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji,
Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya
iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.
Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za
Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe
kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu
ambazo zilitoka nje ya maadili.
“Kuna vipande vitatu ambavyo
kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi,
lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza
chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.
Kabla
ya paparazi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa
huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi
hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa
aendelee.
“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani
pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema
rafiki huyo wa Aunt kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na
bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi
suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent
Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa
na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya
sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.
No comments:
Post a Comment