Kocha wa Taifa Stas, Kim Poulsen amesema anaamini kikosi chake
bado kina nafasi ya kusonga mbele kwenye harakati hizo za kuwania kufuzu
kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Harakati za Stars kusaka tiketi ya kwenda Brazil zimepunguzwa kasi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Morocco, huku wapinzani wake Ivory Coast wakishinda 3-1 dhidi ya Gambia na kuweka kibindoni pointi 10 mwishoni mwa wiki. Akizungumza na Mwananchi baada ya mechi hiyo Kim alisema siku zote malengo ya Taifa Stars ni ushindi na kusonga mbele kwenye michuano hii.

Ikiwa Stars itaifunga Ivory Coast, itafikisha
pointi 9 na itabidi iombe Ivory Coast wapoteze mechi yao ya mwisho dhidi
ya Morocco ili wao waifunge Gambia na kuingia raundi ya tatu.
Katika mchezo wa Taifa Stars dhidi Morocco, bao la Stars lilifungwa na Amri Kiemba katika dakika ya 61, huku yale ya Morocco yakifungwa na Abderazzak Hamed Allah (37) na Youssef El Arabi(50). Stars inategemewa kuwasili leo alfajiri tayari kujiandaa na mechi muhimu dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati huohuo; Kiungo wa zamani ya Yanga, Godfrey
Bonny amesema kocha Kim bado ana nafasi ya kuifanya Stars kuwa tishio
kwa vigogo barani Afrika.
Alisema Stars ina kasoro ndogo ndogo kama kocha Kim akizifanyia kazi basi timu hiyo itafanya vizuri.“Kwa sasa timu inafanya vizuri, ukiachilia hujuma iliyosababisha timu kufungwa 2-1 na Morocco juzi usiku, timu inacheza vizuri na ipo katika nafasi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia,” alisema kiungo wa zamani wa Stars, Bonny.
Bonny alisema timu ina washambuliaji wazuri ingawa
upangaji upo chini yake, unaweza kuwa tatizo kwa baadhi ya mechi. “Ni
kweli upangaji, wakati mwingine unakuwa kama karata, kwa mfano juzi,
niliona si sahihi kwa Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa kuanza pamoja
wakati wote ni wakimbizaji.”
“Ulimwengu ni mchezaji mwenye nguvu, tumezoea
kuona akicheza kipindi cha pili baada ya kuusoma mchezo na kuweka mambo
sawa,”alisema Bonny.
No comments:
Post a Comment