EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, June 27, 2013

Watanzania 35 waswekwa gerezani Pakistan

*Watuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya, wizi
*Serikali yahaha kusaka ndugu zao
WIMBI la vitendo vya Watanzania kukimbilia nje ya nchi kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kutafuta maisha, kujificha na kushiriki biashara za magendo, limechukua sura mpya, baada ya raia zaidi ya 35 kukamatwa nchini Pakistan.

Raia hao, ambao wametajwa kwa majina, wameonekana wengi wamezaliwa Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga, huku umri wao wa kuzaliwa ukiwa kati ya  1957 hadi 1983, wamewekwa katika magereza mawili ya Lahore na Rawalpindi, nchini Pakistan.

Taarifa iliyotolewa juzi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, ilisema Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na kujihusisha na makosa mbalimbali.

Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Buruhani, amesema kuwa Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na makosa mbalimbali, yakiwamo ya kukutwa na dawa za kulevya, wizi wa mali za umma, kuishi Pakistan bila kibali na kutokuwa na hati za kusafiria.

“Katika taarifa yetu ya awali hatukutoa sababu, lakini kutokana na kuhojiwa na waandishi wengi tumelazimika kutoa sababu ambapo tuliwataka wazazi, ndugu na jamaa wajitokeze hapa kwetu ili watoe ushirikiano kwa lengo la kufanikisha kuwarejesha nchini.“Raia hawa walianza kwenda nchini Pakistan kuanzia miaka ya 1989 na hujulikana ni raia wa Tanzania, baada ya kufanya makosa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kwa hawa raia walio katika magereza hayo, walihukumiwa kuanzia miaka ya 2003 hadi mwaka jana, wengine wamemaliza vifungo vyao hivyo hawawezi kuachiwa mpaka wakabidhiwe kwenye nchi husika.

“Hawa wanaotakiwa kurudishwa nchini, ni wale waliomaliza kutumikia vifungo vyao, kuna wengi walihukumiwa kulipa faini, lakini kutokana na kutokuwa na ndugu, walitumikia kifungo.

“Tumechunguza umri wao na miaka waliyokaa huko, tumegundua walikwenda wakiwa na umri wa vijana kati ya 25 hadi 30 na biashara yao ilikuwa ni dawa za kulevya, pengine tayari wametengeneza familia isiyo halali nchini humo,” alisema.

Alisema idara yake imeshindwa kuweka mawasiliano ya moja kwa moja na ndugu wa raia wanaoshikiliwa, kwa sababu ya kukwepa usumbufu.

Watanzania wanaoshikiliwa Pakistan ni Usma Mdoe, mzaliwa wa Tanga, Hemed Himji (Dar es Salaam), Mbwana Eka (Zanzibar), Furahisha Seif (Dar es Salaam), Omar Twaha (Mwanza), Alamgiri Akbar (Dar es Salaam),  Abubakar Khamis (Tanga), Mohamed Abdul (Tanga), Mohamed Mohamed (Tanga) na Ali Kipuya (Dar).

Wengine ni Ashraf Zakhy (Tanga), Mwinyi Mwinyigoha (Pwani), Athuman Singano (Tanga), Abubakar Ally (Zanzibar), Said Mohamed (Dar es Salaam), Omar Suleiman (Pwani), Abdullah Rayngul (Lindi), Jamal Jaffar (Dar es Salaam), Frank Kimweri (Dar es Salaam), Rajab Simbaulaya (Dar es Salaam), Hafdh Sharif (Tanga), Juma Chonanga (Dar).

Pia wamo, Mohamed Juma (Zanzibar), Hassan Mohamed (Dar es Salaam), Bonane Dilunga (Dar es Salaam), Rajab Msalagala (Tanga), Mansoor Kaswamba (Dar es Salaam), Ally Said (Tanga), Mohamed Bashiri (Dar es Salaam), Uruka Malipula (Morogoro), Seif Seif (Zanzibar), Shaaban Mussa (Dar es Salaam), Said  Madelelia na  Rashid Sambatora (Dar es Salaam).

Alisema Watanzania wamekuwa na tabia kukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta maisha, bila kufuata taratibu zinazotakiwa.

Alisema wengi wao, wamekuwa na tabia ya kukimbilia nchi za Afrika Kusini, Pakistan, Botswana na nchi nyingine ambazo ni jirani.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate