KLABU ya Arsenal baada ya kumalizana kwa
dau la Pauni Milioni 22 na Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid, sasa
inahamishia nguvu zake kwa mshambuliaji wa Manchester United, anayeuzwa
Pauni Milioni 20, Wayne Rooney - huku kocha Arsene Wenger akiwa
amedhamiria kuendelea kumtumia katika nafasi ya kiungo mshambuliaji
nyuma ya Muargentina huyo.
Higuain ni mchezaji ambaye Arsenal sasa
wana uhakika wa kumnasa, huku Carlo Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao
wa Hispania, akitarajiwa kutua leo kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji
huyo Bernabeu.
Lakini katika uhamisho huo wa Rooney,
Arsenal italazimika kumlipa mshahara wake wa Pauni 220,000 kwa wiki,
ambao ni mkubwa mno kulingana na tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu
'bakhili'.
Wenger haoni kama Rooney ni mshambuliaji
wa kati, lakini kama kiunganishi, baina ya kiungo na Higuain — nafasi
ambayo mchezaji mwenyewe amesema inamfaa.
Lakini Chelsea pia inamtaka Rooney na
kocha mpya wa United, David Moyes anatarajiwa kukutana na Rooney wiki
mbili zijazo, hivyo uwezekano wa yeye kujiunga na klabu hiyo ya London
bado mdogo.
United haitataka kumuuza Rooney kwa
Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa washindani wao wakuu katika mbio za
ubingwa na matumaini ya mchezaji huyo yanabakia katika kikao chake na
Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo mpya mzuri Old Trafford, hususan
baada ya klabu kusema hajawahi kuomba kuondoka United.
Hilo ni suala lililotokana na wasiwasi
wa Rooney juu ya uhusiano wake na mashabiki wa United. Rooney anatarajia
kikao kama alichowahi kufanya na kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson
mwishoni mwa msimu uliopita, cha binafasi kujadili mustakabali wake
katika klabu.
Arsenal imetenga bajeti ya kutosha
kupambana katoka soko la usajili, lakini tatizo ni kwamba wataweza
kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa sababu ni wenye kiu ya mataji,
vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo vimekuwa adimu.
Mzee wa matarajio: Arsene Wenger wa Arsenal yuko tayari kugombea saini ya Rooney.
No comments:
Post a Comment