Uongozi wa klabu ya Yanga siku ya jana umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea
na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema
uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya
kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama
klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za
kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi
wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona
ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya
kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari:
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier
League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo
Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake
kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam
Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam
Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika
misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi
iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi
iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka
huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia
kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi
kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu
inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo
zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
2.2 Mfumo
(undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha
mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na
Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya
Tanzania.
2.3 Makubalianokati
ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba
Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya
Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii,
ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye
ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya
timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati
ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato
ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho
katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1 Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa
Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL
na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni
ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya
utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka
“matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam
F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na
msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya
mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa
YANGA.
3.3 Azam
na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA
alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya
Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama
Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba
wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao
badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya
habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu
fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za
kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu
wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na
TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA
kufanya ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA
5.1 Mamlaka
ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu
(Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA.
TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya
kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock,
stock and barrel."
5.2 TPL
inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya
mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya
udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu
urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi
ya uhusiano na hivyo
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano,
moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya
mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa
michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es
Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila
mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za
YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni
8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya
TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma
kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau
wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana
kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya
Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara
yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo
makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya
Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo
wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA
linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu
vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam
Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo
wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
No comments:
Post a Comment