JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imemuonya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kuacha matamshi
ya kichochezi yanayoweza kuleta mgawanyiko.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alitoa kauli hiyo jana
wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika huko Micheweni Mkoa
wa Kaskazini Pemba na kusema Maalim Seif anatakiwa kukubali kufanya
kazi chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) au ajiuzulu.
Shaka alisema anachokitafuta Maalim Seif ni kutokea kwa mpasuko
katika SUK kabla ya mwaka 2015 kwa kuamini hata akigombea kwa mara ya
tano hatapata ushindi.
Alisema Maalim Seif anaposema anabaguliwa na hashirikishwi katika SUK
Zanzibar, ni dhahiri anakusudia kutokee ghasia, mpasuko na mkorogano,
ili Zanzibar irejee katika mivutano iliyokuwepo mwaka 1995 na
kusababisha watu kupoteza maisha.
Aidha, mtendaji huyo wa UVCCM Zanzibar alimtaka Maalm Seif kuacha
kumsakama Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd kwa hoja zisizo
na msingi katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kitendo chochote cha Maalim Seif kitakachoashiria kumpaka matope Balozi Seif, UVCCM haitakaa kimya na kuacha atambe.
Alimtaka makamu huyo wa kwanza wa rais ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF kukubali kukaa pembeni na kuwapisha vijana.
VIA TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment