MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefanyiwa oparesheni ya haraka kwa ajili ya kuondolewa uvimbe tumboni.
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe
huo siku nyingi pasipo kujijua hadi alipougua ghafla wakiwa katika
mizunguko ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Ghafla alibadilika, hakuwa katika hali ya kawaida kwani tulikuwa
tukipiga stori lakini nikashangaa mwenzangu anabadilika kama mtu
aliyepandwa na presha hivi.
“Tulilazimika
kuahirisha misele yetu, ikabidi twende Hospitali ya Aga Khan na ndipo
alipogundulika kuwa ana uvimbe tumboni kisha kufanyiwa upasuaji haraka
sana kwani ulikuwa katika hatua mbaya za kuleta madhara,” kilisema
chanzo hicho.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema staa huyo anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment