Baadhi
ya askari wa Jeshi la Polisi wakiangalia Buti Ndefu ya ngozi(Long
Boot)iliyotengenezwa maalum kwa ajili ya askari katika Kiwanda cha Jeshi
la Magereza kilichopo Gereza Karanga, Moshi. Askari hao wametembelea
Banda la Maonesho ya Nanenane la Jeshi la Magereza leo Agosti 02, 2013
lililopo Nzuguni, Dodoma ambapo wamepongeza ubora wa bidhaa mbalimbali
zilizopo katika Banda la Jeshi la Magereza.
Jeshi la Magereza Nchini katika kutekeleza
jukumu lake la kuwalinda na kuwarekebisha wafungwa huwapatia pia mbinu
na stadi za ufungaji bora ili waweze kuitumia katika Jamii zao pindi
wamalizapo vifungo vyao.
Aina ya mifugo inayofugwa na Jeshi la Magereza ni ng'ombe wa nyama na maziwa, mbuzi wa kienyeji na wa maziwa, kondoo, nguruwe, sungula, simbilisi, kuku wa nyama, kuku wa mayai, bata wa weupe na wa kienyeji.
Mazao yatokanayo na mifugo kama nyama na
maziwa hutumika kulisha wafungwa na ziada huuzwa kwa askari na Wananchi
waishio jirani na mashamba hayo. Aidha mifugo hai huuzwa kwa Wananchi
mbalimbali wanaohitaji kufuga na samadi hutumika kurutubisha ardhi ya
Jeshi la Magereza kwa ajili ya Kilimo na ngozi huuzwa katika Viwanda vya
ngozi hapa Nchini.Aina ya mifugo inayofugwa na Jeshi la Magereza ni ng'ombe wa nyama na maziwa, mbuzi wa kienyeji na wa maziwa, kondoo, nguruwe, sungula, simbilisi, kuku wa nyama, kuku wa mayai, bata wa weupe na wa kienyeji.
Akizungumzia baadhi ya Changamoto zinazoikabili Sekta ya Ufugaji Mifugo hapa nchini, Mtaalam wa Mifugo katika Banda la Maonesho ya Nanenane la Jeshi la Magereza, Stafu Sajini Charles Masuka alisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na upatikanaji mdogo wa maji ambapo mabwabwa ya maji yaliyopo hayakidhi mahitaji ya wafugaji wengi hapa nchini hali inayowafanya wafugaji wengi kufuga kwa kuhamahama.
Pili, magonjwa ya milipuko ambayo yanatokomezwa kwa njia ya chanjo ambapo wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kubwa kwani milipuko ya magonjwa ya mifugo inapotokea mifugo mingi hufa.
Changamoto nyingine ni wavamizi katika maeneo ya malisho hali ambayo inasababisha migogoro ya mara kwa mara ya kugombania maeneo ya malisho ya mifugo pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo husababisha ukame katika maeneo mbalimbali hivyo kukosekana kwa malisho ya kutosha kwa mifugo.
"Wito wangu kwa Serikali ni kuwa waandae mpango mahususi wa kuwachimbia wafugaji mabwabwa ya kutosha kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua pamoja na kuandaa programu za chanjo ya mifugo kila mwaka ili kuyatokomeza magonjwa mbalimbali ya milipuko". Alisema Stafu Sajini Charles.
Miongoni mwa mashamba makubwa yanayofuga ng'ombe wa nyama na maziwa ni pamoja na Gereza Ubena - Pwani, Mbigiri- Morogoro, Mugumu - Mara, Kitengule - Kagera, Kingurungudwa na Kilwa - Lindi, Namajani - Mtwara, Majimaji - Ruvuma na King'ang'a - Dodoma. Aidha, Mikoa yote nchini kuna Magereza yanayofuga idadi ndogo ya ngo'mbe wa nyama na maziwa kwa ajili ya nyama ya kulishwa wafungwa, ziada huuziwa askari na raia.
NA:Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Dodoma
No comments:
Post a Comment