ULE mwaliko uliobuma wa mastaa wa Bongo Muvi wa kwenda kufuturu ikulu na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
umeibua tafrani na kusababisha moto kuwaka ndani ya tasnia hiyo.
Baadhi
ya mastaa hao wanatuhumiana kutapeliana fedha walizochangisha kwa ajili
ya kukodi magari ambayo yangewabeba kutoka pale Viwanja vya Leaders,
Kinondoni hadi ikulu iliyopo Magogoni, Dar.
Akizungumza na gazeti
hili kwa sharti la kutotajwa, mmoja wa wasanii hao alisema: “Baada ya
kukusanyika pale Leaders (siku ya tukio) tuliamua kuchangishana kwa
ajili ya kukodi magari ambayo yangetupeleka ikulu lakini wakati zoezi
hilo likiendelea ndipo ulipokuja ujumbe kuwa safari hiyo imekufa baada
ya Rais Kikwete kupata mgeni kutoka Marekani, Bill Clinton.
“Sikuwa
na shaka na taarifa zile za kuahirishwa kwa mwaliko wa kwenda kufuturu
ikulu, nilitegemea kuwa kila mtu aliyechangishwa angerudishiwa fedha
zake lakini hadi tunaondoka maeneo ya Leaders hakuna aliyerudishiwa.”
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta aliyekuwa mratibu
mkuu wa mwaliko huo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo aliposomewa
mashtaka yake alikiri kutokea matatizo hayo huku akitupa lawama moja kwa
moja kwa wachangishaji.
“Muulize Muhogo Mchungu (Rajab Mkumbila) au Chiki (Salum) Mchoma, hao ndiyo watakupa jibu kamili,” alisema Steve Nyerere.
“Muulize Muhogo Mchungu (Rajab Mkumbila) au Chiki (Salum) Mchoma, hao ndiyo watakupa jibu kamili,” alisema Steve Nyerere.
Credit: GLP
Kwa upande wake, Chiki alisema kuwa hapendi kuzungumzia suala hilo huku
naye akimtupia mpira Muhogo Mchungu kuwa ndiye aliyekuwa na daftari la
waliochangisha.
Naye Muhogo Mchungu alipotafutwa na mwanahabari wetu alisema kuwa kama kuna mtu anadai fedha zake amtafute na si kulalamika kwenye vyombo vya habari.
Naye Muhogo Mchungu alipotafutwa na mwanahabari wetu alisema kuwa kama kuna mtu anadai fedha zake amtafute na si kulalamika kwenye vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment