Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarajiwa kuhutubia
waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za
majeruhi .
Inasemekana kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la
kuondokea na kuingilia wageni.Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari
watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa na baadhi ya operesheni za
uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo
zikielekezwa kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es
Salam ,Kigali, Mombasa na kwingineko nchini Kenya.
Wakati huo huo star wa muziki Bongo Diamond ameshuhudia kila kitu wakati
akijiandaa kurejea Bongo baada ya kuwepo Kenya kwa ajili ya kubadilisha
ndege akitokea nchini Afrika Kusini.
Kupitia website yake ya This is Diamond amesimulia ilivyokuwa,shuka nayo..
Hapa unapo paona ndo hali ilivyokuwa majira ya saa 1 asubuhii ndani ya Nairobi....
Niliwasili Alfajiri ya saa kumi na moja nikitokea nchini South Africa
nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini
maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi
na abiria wengine tukisubiri kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya
usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege
ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto....
Hadi sasa sasa chanzo cha moto ule uliosababisha kuwaka kwa Airport bado sijajua lakini
hii imepelekea safari kukwama,sina uhakika kama tutaweza kuja Dar tena au Ndege
kama zitaweza kuruka kwa leo maana hapa tulipo wanatupeleka hotelini,
Imewalazimu Uongozi wa Immigration kuja na kutugonga mihuri kwenye basi
la wasafiri na kuwekewa usalama wa mabegi yetu....
Zifuatazo ni Picha za Tukio zima Pale Airport ya Nairobi.....!!






No comments:
Post a Comment