KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa, amewaasa Watanzania kutambua kuwa Katiba ni uhai wa
taifa, hivyo wawe huru kutoa maoni ili baadaye iwatetee na kuwalinda.
Dk. Slaa alisema hayo katika mkutano wa kukusanya maoni ya Katiba
mpya uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini hapa juzi.
Katika mkutano huo maelfu ya wananchi walikusanyika kutoa maoni ya Katiba mpya.
Alisema chama chake kimeamua kukusanya maoni kwani Katiba si mali ya
chama, bali ni ya Watanzania wenyewe hivyo wameona ni vema kuwakusanya
kwa pamoja kutoa maoni yao ambayo ni haki ya kila Mtanzania.
Dk. Slaa alisema wenye mawazo ya kufanana wana uwezo wa kutengeneza
Katiba itakayowalinda na wala si itakayolinda chama chochote cha siasa
Alisema Katiba iliyopo inatumiwa vibaya na viongozi walioko madarakani
kwa sababu wale wanaouvunja maadili kwa kuiba rasilimali za umma
hawachuliwi hatua.
Akizungumza zaidi katika mkutano huo alisema serikali tatu itapunguza
gharama za uendeshaji kwa kuokoa fedha nyingi kwani asilimia ya wabunge
na mawaziri itapungua kwa kiasi kikubwa.
Pia aliwata Watanzania kuacha woga katika kudai haki kwani kufanya hivyo ni kutojitendea haki, hata Mungu anakataza.
Naye mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA, Mabere Marando, alisema
watahakikisha wanawafikia Watanzania na kuwaelewesha Rasimu ya Katiba
Mpya na msimamo wa chama hicho.
Hata hivyo alisema chama hicho kitawafikia wananchi katika maeneo yao
kuwaelewesha na kupata maoni, hivyo ni vema kusema nini wanataka kiwemo
katika Katiba hiyo mpya.
Credit: Tanzania Daima.
No comments:
Post a Comment