
Wanamgambo wa kundi la Al Qaeda linaloitishia Marekani 
                  
Marekani inasema itaendelea kufunga balozi zake Kaskazini mwa
 Afrika na Mashariki ya kati hadi siku ya Jumamosi kwa hofu ya 
kushambuliwa na Al-Qeada.
Balozi 21 zimefungwa tangu Jumapili baada ya wizara ya mambo ya
 nje ya Marekani kutangaza kuwa kundi la Al Qaeda lilikuwa linajiandaa 
kufanya mashambulizi.
Marekani imewataka raia wake kuepuka kusafiri Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati hadi pale watakapopewa maelezo zaidi.
Hata hivyo Marekani imesema kuwa itafungua balozi zake nchini Algeria, Afghanistan na Iraq jana Jumatatu.
Uingereza nayo imejiunga na Marekani kufunga ubalozi wake jijini 
Sanaa nchini Yemen na kusema kuwa utafunguliwa baada ya kumalizika kwa 
kipindi cha Ramadhani.
Mbali na Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, Marekani imeongeza 
kuwa balozi zake jijini Antananarivo nchini Madagascar, Bujumbura, 
Djibouti, Khartoum, Kigali na Port Louis nchini Mauritius zitafungwa 
wiki hii.
No comments:
Post a Comment