WATU watano wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa baada ya
gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupasuka gurudumu la nyuma
huko Fukayosi barabara ya Kiwangwa/Bagamoyo, wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa
Pwani.
Tukio hilo limetokea jana saa 12 asubuhi wakati gari namba T 123 CGU
aina ya Toyota NOAH likiendeshwa na Shaban Muharami (38) lilipokuwa
likitokea Kiwangwa kwenda Bagamoyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alithibitisha kutokea
kwa ajali hiyo na kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joyce Mkahe (23)
mkazi wa Kiwangwa, Haji Makame (33), mkazi wa Kiwangwa Bagamoyo, Doto
Maulidi (31), mkazi wa Boko, Amina Mshomi (32) mkazi wa Kiwangwa na
Hassan Athuman (31) mkazi wa Kiwangwa Bagamoyo.
Aliwataja majeruhi kuwa ni Omari Ramadhan (35), Melekzedek Urio (32),
Tatu Athuman (32) na Abdul Hamis (42) wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo.
Alisema kutokana na hali yao kuwa mbaya majeruhi hao walihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Majeruhi wengine ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya
Bagamoyo ni Juma Nasoro (34) mkazi wa Sanzale Bagamoyo; Alfred Andrew
(29) mkazi wa Kiwangwa; na Paulina Andrew (33) mkazi wa Kiwangwa huku
dereva wa gari hilo akishikiliwa na polisi
No comments:
Post a Comment