WINGA
mpya wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), jana amejiunga rasmi na kikosi
chake hicho zikiwa ni siku chache baada ya kumaliza majukumu yake Taifa
Stars, lakini akaeleza kile anachoamini ndiyo sahihi katika sakata lake
la kusajiliwa na timu mbili.
Msimu uliopita, Ngassa aliitumikia
Simba kwa mkopo akitokea Azam, lakini Simba imekuwa ikidai iliingia naye
mkataba wa mwaka mmoja, uliotarajiwa kuanza baada ya ule wa mkopo
kumalizika, suala ambalo winga huyo amekuwa akilipinga.
Winga huyo hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili na Yanga.
CREDIT: GLP
No comments:
Post a Comment