Habari na Tanzania Dima
MASHINE ya Magnetic Resonance Ination (MRI) inayotumika kupima
magonjwa mbalimbali katika mfumo wa fahamu imeharibika kwa zaidi ya siku
nne na kusababisha usumbufu mkubwa.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa wagonjwa wengi
waliohitaji huduma hiyo wameshindwa kuipata kutokana na kuharibika kwa
kifaa hicho muhimu cha kupima na kutambua magonjwa mbalimbali katika
ubongo, uti wa mgongo na kifua.
Akizungumza kwa niaba ya mgonjwa wake, Joshua Shaka, alisema kuwa
wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma hiyo kwa siku nne mfululizo bila
mafanikio baada ya kuelezwa kuwa mashine hiyo imeharibika.
Alisema kuwa kuna umuhimu wa serikali kuangalia namna ya kuagiza
mashine mpya kwa kuwa iliyopo imekuwa ikiharibika mara kwa mara.
“Hii mashine sio mara ya kwanza kuharibika; unaweza kuja leo ukaambiwa
inafanya kazi lakini baada ya muda mfupi inashindwa kuendelea na kazi
…inawezekana ni kutokana na uchakafu,” alisema.
Alisema kuwa mashine hiyo ndiyo inayotoa huduma kwa hospitali zote za
serikali kwa jiji zima la Dar es Salaam hivyo hatua ya kuharibika mara
kwa mara imekuwa ikisababisha kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa
wanaohitaji huduma hiyo.
“Hata hiyo mashine ya CT SCAN inayosemekana ipo hivi sasa nayo haina
filimu hivyo unapopigwa unashindwa kupewa majibu hapo hapo jambo
linalozidi kumfanya mgonjwa azidi kuumwa zaidi maana anategemea aje
hospitali apate huduma,” alisema.
Tanzania Daima Jumamosi, katika uchunguzi wake, lilidhihirishiwa
uharibifu wa mashine hiyo na baadhi ya wahudumu waliokutwa hospitalini
hapo.
“Mashine ni mbovu kama mnataka huduma labda mniache simu zenu kama
itapona wiki ijayo nitawapigia ili muweze kumleta mgonjwa wenu kuliko
mje tena mkute mashine haifanyi kazi mtakuwa mnamchosha mgonjwa wenu
bure,” alisema mmoja wa wahudumu waliokuwepo.
Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha, hakupatikana
baada ya ofisi yake kufungwa kwa muda mrefu, na hata alipotafutwa kwa
njia ya simu yake ya kiganjani nayo iliita mara nyingi na kwa muda mrefu
bila majibu.
Hata hivyo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris
Mwamaja, alikiri kuharibika kwa mashine hiyo na kusema kuwa wamemaliza
kukitengeneza jana na kwa sasa kinafanyakazi.
No comments:
Post a Comment