Watu wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana
Jumatatu walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano
wa 'sausage' karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya
Darajani mjini Zanzibar.
Msaidizi wa
Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis
Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu
taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa
kazini kwenye
Duka la Sahara, aliona idadi
ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea
Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na
walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti
upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa
mbele ya duka hilo.
"...lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku," alisema Mkadam (tizama video iliyopachikwa hapo chini kutoka kwa Munir Zakaria) akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye.
Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.
Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa.

No comments:
Post a Comment