EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 24, 2013

KILICHOIPONZA FAMILIA HII NI HIKI..MAUAJI ya watu watatu wa familia moja.

Stori: Mashaka Baltazar, Mwanza
MAUAJI ya watu watatu wa familia moja yaliyotokea jijini Mwanza hivi karibuni yameibua maswali mengi lakini mwisho wa yote, imebainika kuwa kilichoiponza familia hiyo kukumbwa na mauti hayo ni hiki, Uwazi limechimba mwanzo mwisho.
Mauaji hayo yalitokea saa 10 alfajiri ya Septemba 21, mwaka huu katika Kijiji cha Ihila, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo inaaminika kuwa mgeni aliyekaribishwa kwenye familia hiyo ndiye aliyetekeleza mauaji hayo na alikaribishwa nyumbani hapo bila kujulikana tabia.
Debora Jonas Luhinga, mtoto wa marehemu ambaye alinusurika katika tukio hilo, alisema kuwa mgeni huyo aliyemfahamu kwa jina moja la Lameck alifika nyumbani hapo Septemba 18, mwaka huu lakini baada ya kutekeleza mauaji hayo alitokomea kusikojulikana.
Debora mwenye umri wa miaka 12, alidai kuwa siku ya tukio, usiku akiwa amelala, mdogo wake aitwaye  Eliudi aliyekuwa amelala naye aliamka na kuanza kulia sana.
Alisema  alichukua jukumu la kumbembeleza mdogo wake huyo lakini ilishindikana, ghafla Lameck aliingia chumbani humo na kumwomba mtoto huyo ili ampeleke chumbani kwa wazazi wake akabembelezwe.

“Kilio cha mdogo wangu kilikuwa kikubwa, mara nikaona mlango unafunguliwa, Lameck akaingia, akasema kwa kuwa mtoto analia sana nimpe ampeleke kwa mama ili akambembeleze,” alisema Debora.
Akaongeza kuwa alikubali kumpa Lameck mtoto huyo na kwa vile yeye alikuwa na usingizi mzito aliendelea kulala fofofo.
Debora alisema alipoamka kulikuwa kumekucha, akashuka kitandani ili aende nje lakini akakuta mlango umefungwa kwa nje.
“Nilipiga kelele baada ya kukuta mlango wa chumba changu umefungwa kwa nje, majirani walifika kunifungulia lakini nilipigwa na mshangao kukuta maiti ya baba ikiwa sakafuni sebuleni tena imetapakaa damu.
“Nikiwa nimechanganyikiwa niliingia chumbani kwa wazazi wangu, nikashangaa kumuona mama yangu na mdogo wangu Eliudi  wakiwa wameuawa kwa kunyongwa na miili yao imelazwa chini,” alisema Debora.
Debora alisema anaamini Lameck ambaye mara nyingi alikuwa akimwona akizungumza na baba yake ndiye aliyetenda unyama huo. Alisema anaamini mtu huyo wakati anaingia chumbani kwake kumchukua mdogo wake alikuwa ameshawaua wazazi wake na aliamua kumtwaa mtoto huyo kwenda kumnyonga ili kilio chake kisiwafanye majirani wakafika nyumbani hapo kutaka kujua kulikoni na hivyo kugundulika alichokifanya kwa muda huo.
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema anaamini baba yake ndiye aliyeanza kuchinjwa kabla ya  mama yake kunyongwa.
Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili huku wakiomba majina yao kuhifadhiwa baada ya tukio hilo, walisema kwa nyakati tofauti kuwa huenda mauaji hayo ni ya kulipiza kisasi kwa mwanaume huyo ila mkewe na mtoto waliingizwa kwenye mkumbo tu.
Walisema haiwezekani watu wa familia moja wakauawa kikatili namna hiyo bila ya wauaji kuanika sababu.
Waliongeza kwa kudai kuwa siku zote tatu alizoishi hapo, Lameck alikuwa akitafuta njia mwafaka ya kutekeleza ukatili huo.
Walisema  mauaji mengi ya aina hiyo yanayotokea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza huhusishwa na imani za kishirikina, migogoro ya ardhi au mirathi.
Majirani hao waliongeza kuwa awali walikuwa wakimwona Lameck nyumbani kwa marehemu bila kujua uhusiano wao, wakaonya kuwa ni hatari sana kumkaribisha nyumbani mtu usiyemjua kwa undani kama ilivyokuwa kwa Lameck.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema hakuna aliyekamatwa. Aliwataja marehemu kuwa ni Jonas Luhinga, mkewe Rusia Jonas na mtoto wao, Eliud Jonas.
CHANZO NI GLP

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate