NA IRENE MWAMFUPE NDAUKA.
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE....Baba Joy alitingisha kichwa kama kukubaliana na maneno
ya
Fuko...
”Oke...sawa, ni nimekuelewa vizuri, endelea na kazi,”
alisema baba Joy.
Alisimama mlango mkubwa na kumwita mkewe...
”Mama Joy...”
”Abee.”
Sekunde kadhaa mbele, mama Joy alisimama mbele ya
mumewe...
”Abee...”
”Hili fuko la taka hapa chafuchafu vipi?”
“Siii,” alimwita
maana alikuwa amempa mgongo akielekea kona nyingine ya nyumba.
Mama Joy aligeuka na
kumwona mzoa taka, akaachia tabasamu laini…
“Wewe umezamaje humo
ndani..?”
“Nimezama tu
mwenyewe, si unajua tena kujiokoa…”
“Haya toka tuongee
sasa, maana pale ulimuulizia yule kijana ni nani, yule kijana anaitwa Bonny, ni
kijana wa nyumba ya tatu tu hapo mbele, familia yake na familia yangu ni kama
marafiki wakubwa sana, alikuja kunisalimia,” alisema mama Joy baada ya mzoa
taka kutoka katika dude la kuzolea taka…
“Mbona mlinzi wako alisema yeye ni
kama mimi…”
“Yule mlinzi hana akili nzuri, sisi
wenyewe tumemgundua baada ya kuanza kazi, hapa tulipo tunatafuta mlinzi
mwingine,” mama Joy aliamua kumsilibia Fuko akiamini hata yeye Fuko maneno yake
alilenga kumharibia.
Mama Joy kwa wakati huo hakuwa
anahitaji penzi, Bonny alishamgalaza kila mahali, mwili ulikuwa umechoka kama
mtu aliyetoka kufanya mazoezi ya viungo…
“Kwa hiyo sasa?” aliuliza mzoa taka…
“We zoa taka zako nenda uje kesho,
mimi nataka kulala sasa, mwili wote unauma.”
“Unauma kwa sababu gani..?”
“Mzee wako usiku alinikamua sana…”’
“Siyo yule kijana..?”
“Nimekwambia yule kijana ni mtoto wa
jirani, hujaamini tu…”
“Sawa, lakini sasa mimi leo nimekuja
nina shida moja…”
“Shida gani..?”
“Nataka kupanga chumba Manzese…”
“Kwa hiyo unataka pesa za pango..?”
“Eee…”
“Tena itakuwa afadhali, kule nikija
tunajificha zetu. Ni shilingi ngapi?”
“Elfu sitini…”
“Kwa siku moja?” aliuliza kwa
mshangao mama Joy…
“Hapana, kwa miezi sita…”
“He! Ina maana kuna wenye nyumba
wanaochukua kodi ya miezi sita..?”
“Manzese wapo wengi, kama huyu
ninayekwambia.”
Mama Joy alimtaka mzoa taka asuburi
palepale alipo. Aliingia ndani na kutoka na shilingi laki moja na elfu
ishirini…
“Hizi ni kwa ajili ya mwaka mmoja…”
“Eh! Atakubali..?”
“Ina maana huwa hawakubali kupokea
fedha ya mwaka mzima, ajabu!”
Mzoa taka alizipokea, akaondoka
akiahidi kurudi na majibu kesho yake.
***
Usiku wa siku hiyo, mama Joy na
mumewe wakiwa kitandani, mazungumzo yao yalikuwa hivi…
“Mama Joy…”
“Abee,” mama Joy licha ya kuitika
lakini pia mapigo ya moyo wake yalikwenda kwa kasi, haikuwa kawaida ya mumewe
kumwita hivyo usiku wakiwa wamelala.
Hata pale ilipotokea mume anataka
haki yake ya tendo la ndoa alimshika mahali na kumwonesha ishara kwamba
alitakiwa kugeukia upande wa pili sasa…
“Hivi unavyoamini wewe ni mke wa
mtu..?”
“Naamini hivyo, kwani vipi baba Joy…”
“Mimi siamini…”
“Kwa kutumia kigezo gani..?”
“Leo sitakamwabia natumia kigezo
gani, ila kesho au keshokutwa nitakwambia na utakijua tu.”
Mama Joy alionesha dalili za
kumdharau mume wake, akageukia ukutani na kunyamaza kimya.
Baba Joy alilala akiangalia juu,
yaani chali, viganja vya mikono aliviweka kwenye mto na kuegemeza kisogo chake
hapo.
Alikuwa akiamini mkewe ana uhusiano
na mzoa taka na aliendelea kuamini kwamba, jana yake aliporudi kutoka Arusha
kijana huyo alifichwa au alitolewa nje ya nyumba hiyo kwa staili ya kikomandoo…
“Lakini kama ni hivyo, tatizo liko
getini, lazima…”
“Dawa hapa ni moja tu, kumwaga
‘mapesa’, nimmwagie pesa mlinzi, nimmwagie pesa Helana, wao ndiyo watakuwa
wakinipa hatua kwa hatua kwa sababu lazima wanajua,” aliwaza moyoni mwake
baba Joy, hata
alipopitiwa na usingizi hakujua zaidi ya kujikuta ameamka kumekucha lakini
akiwa amechoka sana...
“Leo lazima kila kitu kiwe wazi,”
alisema akitoka chumbani akiwa na pajama mpaka jikoni ambako alimkuta Helena
akifanya usafi…
“Hujambo Helena…”
“Sijambo bosi, umeamkaje?”
“Mimi mzima. Eee, nina shida na wewe,
lakini iwe siri ya sisi wawili…”
“Ipi tena hiyo bosi?” aliuliza
Helena. Akilini aliwaza kwamba, neno litakalotoka kwenye kinywa cha baba Joy
ni…
“Mimi nimetokea kukupenda sana, sasa
kwa sababu mama Joy analeta mambo ya kijinga naomba sana uwe mpenzi wangu,
lakini tufanye kwa siri.”
Lakini kilichotoka kinywani mwa baba
Joy ni hiki…
“Najua mzoa taka bado anaingia…na
najua kwamba anapoingia wewe huwa unaona kwa macho yako. Sasa nataka nikupe
pesa, lengo langu akiingia tu, unibip kwa simu, sawa?”
“Sawa bosi, lini…?”
“Leo, kesho, keshokutwa, yaani akija
tu…”
“Sawa bosi…”
“Unataka shilingi ngapi?” baba Joy
alimuuliza Helena huku akiwa amemkazia jicho la kusikiliza…
“Mh! Bosi, mimi nadhani angalia wewe
mwenyewe kiasi utakachotaka kunipa sawa tu kwangu.”
“Oke, nikiwa natoka kwenda kazini
nitakupa mzigo wako.”
“Sawa bosi.”
Baba Joy aliondoka hadi getini…
“Fuko…”
“Shikamoo bosi…”
“Achana na shikamoo, nataka tuongee…”
“Sawa bosi…”
“Naamini mzoa taka anapoingia wewe
huwa unakuwa getini?”
“Ni kweli bosi, lakini…”
“Sitaki kujitetea, subiri nimalize
ninachotaka kuongea…”
“Sawa bosi…”
“Nitakupa pesa, ninachotaka ni
kwamba, akiingia tu, unanibipu…”
“Tena leo lazima atakuja bosi…”
“Una uhakika..?”
“Ndiyo bosi…”
“Oke, basi mimi nitakapotoka,
nitajifanya nakwenda ofisini, lakini sitafika huko, nitakuwa jirani tu…”
“Sawa bosi.”
Baba Joy alirejea ndani, chumbani,
akaenda kuoga. Wakati anaoga mama Joy aliamka na kutoka. Alianzia jikoni na
baadaye uani. Alikuwa hajui hili wala lile…
“Nimemmisi mzoa taka wangu. Kale
kakijana sijui kanatumia mzizi, nakapenda sana kuliko mlinzi. Ila Bonny yeye
ana mwili wa mazoezi, amevimbavimba vizuri…teh… teh… teh teh!”
Baba Joy alipomaliza kujiandaa,
alitoka mkononi ameshika brifkesi yake. Alianzia jikoni kwa Helena. Alipofika,
aliweka brifkesi juu ya kabati na kulifungua, akatoa shilingi laki mbili…
“Kamata hizi Helena, nataka kazi
nzuri…”
“Jamani bosi, asante sana, kazi
njema,” alisema Helena huku akipokea kwa kuonesha dalili ya kupiga magoti.
Baada ya baba Joy kuondoka, mama Joy
alitokea jikoni…
“Nimekusikia ukisema jamani bosi,
asante sana, kazi njema, ni kitu gani amekupa?”
Helena alipigwa butwaa, akawaza
haraka na kupata jibu kwamba, kama hakukiona alichopewa, hakuna haja ya
kumtajia…
“Hajanipa kitu…”
“Sasa ulikuwa unashukuru nini..?”
“Alikuwa ameniaga kwamba anakwenda
kazini nibaki salama ndiyo na mimi nikamwambia asante kazi njema.”
Mama Joy alitaka kukubali japo
hakutoa sauti, akatoka kwenda mbele ya nyumba. Ile anatokea, akaona mkono wa
mumewe ukitoka kama kushikana na mlinzi…
“Khaa! Toka lini baba Joy
akasalimiana na mlinzi kwa kushikana mikono?” alijihoji mama Joy, naye akawa
anaelekea usawa uleule. Alifika wakati mumewe akiwa ameshatoka na geti
limeshafungwa na mlinzi…
“Leo baba Joy amekusalimia kwa kukupa
mkono?”
“Ndiyo bosi…”
“Au alikuwa anakupa kitu?”
“Sijakiona bosi…”
“Hujakiona kinini?”
“Hicho kitu ulichosema alinipa.”
Mama Joy akaona kama anaongea na
chizi, akarudi zake ndani na kuendelea na shughuli nyingine za kifamilia.
Mlinzi aliingia ndani ya kibanda
chake na kuzihesabu zile pesa alizopewa na bosi wake…
“Kumi, ishirini, thelathini,
aro…baini, haaamsiniii, sitini, sabini, themanini…” mlinzi alihesabu hadi
alipokoma kwenye noti ya mwisho akiwa anatamka laki mbili…
“Duuu, ole wake aje leo mzoa taka,
kitamnukia. Hii ndiyo mipango ya mjini bwana, kula na wewe uliwe, ala!” alisema
kwa sauti mlinzi licha ya kwamba alikuwa pake yake.
Mara simu ya getini ilipigwa kutokea
ndani, akaiwahi kuipokea…
“Haloo…”
“Fuko, akija mzoa taka mlete ndani
moja kwa moja…”
“Sawasawa bosi.” Simu ikakata…
“Imekula kwako leo, utakiona cha
mtema kuni,” mlinzi alisema moyoni.
Mpaka inatimu saa sita na nusu, mzoa
taka alikuwa hajatokea. Na kwa usongo siku hiyo, kila mara mlinzi alikuwa
akitoka getini na kuangaza kulia na kushoto.
Saa saba, baba Joy alimpigia simu
Helena lakini hakuipokea kwa sababu mama Joy alikuwa beneti…
“We simu yako si inaita, kwa nini
hupokei?”
“Ni msumbufu mtu mwenyewe…”
“Ni nani kwani?”
“Ni mtoto wa baba’angu mkubwa.”
Baba Joy alipoona simu ya Helena
haipokelewi akampigia mlinzi wake…
“Bosi, mzoa taka hajatokea…”
“Ngo ngo ngooo,” geti liligongwa…
“Hebu subiri, geti linagongwa si
ajabu yeye,” alisema mlinzi na kukata simu. Alikwenda kwenye geti dogo na
kufungua akachungulia nje…
“Karibu bwana mzoa taka, karibu
sana,” siku hiyo mlinzi alimchangamkia sana kuliko siku nyingine yoyote ile…
“Asante sana, nimekuja…”
“Eee, najua umekuja, demu wako
alisema ukija nikupeleke mpaka ndani…”
“Demu wangu?”
“Aaa, sasa kwani bosi wangu si demu
wako…”
“Acha hizo wewe, ingia twende,” Fuko
alisema na kumshika mkono kwenda naye. Alipomfikisha ndani, mlinzi alirudi mbio
getini na kuchukua simu yake kumpigia baba Joy…
“Simu unayoipiga kwa sasa
haipatikani, tafadhali jaribu tena baadaye,” simu ilijibu hivyo. Alirudia na
kurudia lakini majibu yakawa hayohayo.
Mara, Helena alitua getini.
“Fuko…”
“Naam…”
“Una namba nyingine ya bosi…?”
“Sina, unamtafuta..?”
“Sikiliza, aliniambia akija mzoa taka
nimpigie simu, yeye hatakuwa mbali na maeneo haya, sasa simpati…”
“Hata mimi hivyohivyo, wewe alikupa
na ‘hela’..?”
“Kwani wewe hajakupa hela..?”
“We nijibu kwanza mimi na mimi
nitakujibu wewe…”
“Hamna, nijibu kwanza wewe,” alisema
Fuko.
Wakati wao wakibishana kama walipewa
fedha au la, mama Joy na mzoa taka walikuwa chumbani, walikaa kitandani
wakisema wanaongea mambo yao…
“Mpenzi, chumba kimepatikana…”
“Wapi..?”
“Kule maeneo ya nanihi, si mbali
sana…”
“Bonge la chumba. Simenti chumba
chote, kikubwa kama uwanja wa mpira, halafu bei ya ubwete…”
USIKOSE SEHEMU YA 10...HAPA
Tuesday, September 24, 2013
CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA...SEHEMU YA 09.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment