BINAFSI nafahamu kwamba Irene Uwoya aliwahi kuwa staa mkubwa nchini
lakini akafanya makosa na sasa ameshuka chati. Ameporomoka kwa kiasi
kikubwa sana.
Elizabeth Michael ‘Lulu’, baada ya ‘ajali’ yake na marehemu Steven
Kanumba, alikaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini baada ya kutoka
ameonekana kuwa na mafanikio makubwa kuliko Uwoya ambaye siku zote yupo
mtaani.
Pengine kuna aina fulani ya maisha ambayo Uwoya
amejichagulia maana akina Rose Ndauka, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na
wengineo wamekuwa wakifanya vizuri, wanamfunika sana. Ameshindwa
kujisahihisha, ataendelea kusugua.
Najua kwamba Uwoya ana hali mbaya
kisanii, amechoka, muonekano wake hausisimui tena, amepoteza mashabiki,
kwa maana hiyo hauzi. Dili za kucheza filamu zinaota mbawa kila kukicha,
maprodyuza wanataka wakali ambao wanafanya biashara sokoni.
Naelewa
kuwa hivi sasa katika ulimwengu wa masupastaa, Uwoya amebaki
msindikizaji lakini sikuwahi kufikiri kwamba anaweza kufikia hatua mbaya
kiasi hicho. Kafikishwa mbaroni kwa wizi wa simu? Yaani wizi wa simu ya
mkononi! Anatia huruma.
Yamemfika yapi? Sitaki kuamini kama Uwoya
anashindwa kununua simu halali. Akili nyingine inaniambia kuwa hawa dada
zetu wanaharibiwa na uchu wa kupenda vitu vya juu lakini uwezo ni
mdogo. Je, huo wizi wenyewe alifanyaje?
Atakapofikishwa mahakamani
pengine itajulikana kama kweli amehusika na wizi huo, basi itafahamika
ameufanyaje. Ni yeye moja kwa moja au kupitia kwa mtu mwingine? Dunia
ina mengi, ni vizuri hili jambo likafika kortini, huko tutajua ukweli
halisi.
Swali langu ni hili, kama kweli ile simu alinunua kwa nini
pale kituoni hakutoa risiti? Hata kama ingekuwa nyumbani, alishindwa
nini kuagiza aletewe kuthibitisha kama ni mali yake? Maswali hayo mawili
yanaongeza uzani kwenye madai kwamba ile simu ni ya wizi.
Ni ya wizi
sawa, je, ni kweli Uwoya anaweza kuiba simu? Inawezekana kabisa akatega
Kariakoo halafu amvizie mtu na kumchomolea? Maana mashtaka dhidi yake
ni Wizi wa Maungoni, yaani wizi wa kumchomolea mtu kitu kutoka mwilini.
Kesi
ipo Msimbazi Polisi na imeandikwa kwenye kitabu cha ripoti za
kumbukumbu (report book ‘RB’) kwa nambari MS/RB/8522/2013. Hata hivyo,
simu yenyewe iliyoibwa ina thamani kubwa, nahisi Uwoya aliinunua kwa mtu
ambaye ndiye mwizi.
Mikono ya Uwoya na vidole vyake vilivyo,
haoneshi kama anaweza kuwa mkali wa kuchomolea watu. Hata kama kaishiwa
na kupigika, siyo rahisi akafanya hivyo. Sura yake haioneshi ushujaa wa
‘kupiga ndole’ lakini ya Mungu mengi.
Labda kauziwa lakini yeye ndiye
kakutwa na mali ya wizi (aliyekutwa na ngozi ndiye aliyeiba ng’ombe).
Kama ipo hivyo, hilo nalo ni tatizo kubwa. Maana yake yeye naye ni mmoja
wa watu wanaowafanya wezi waendelee kufanya uporaji. Anawafadhili kwa
mlango wa nyuma.
Tusimamie hapa kwamba kama alinunua, basi Uwoya ni
mfadhili wa wezi kwa sababu mtu anayenunua mali ya wizi, anawasaidia
wezi kuendelea kuishi kwa uporaji. Kwa maana hiyo siyo mtu mzuri, hafai
kwenye jamii.
Kwa mwenendo huo, naamini ndiyo maana ameporomoka,
anakosa sifa ya kuitwa kioo cha jamii. Inawezekanaje awe mfano wa kuigwa
ikiwa yeye ni kirusi katika hiyohiyo jamii? Mtu unajua kabisa hii mali
ya wizi unainunua kwa bei chee halafu unaona raha.
Kununua mali ya
wizi ni hujuma nzito, ni ukosefu wa huruma kwa sababu wakati wewe
unauziwa mali hizo kwa bei nafuu sawa na bure, halafu unaitumia kwa
nafasi huku ukijionesha, mwenzako anateseka mno.
Fikiria kama wewe
umejibana, ukajitutumua kununua simu aina ya iPhone 5 kwa shilingi
milioni 1.6. Umeitumia wiki mbili tu unaibiwa, halafu mtu mwingine
anakuja kuuziwa kwa shilingi 400,000 au 300,000. Itakuuma kiasi gani?
Bila
shaka utamchukia mwizi na yule aliyeuziwa, kwani angekuwa muungwana
asingekubali kununua. Laiti angekuwa raia mwema, angesaidia huyo muuzaji
akamatwe ili aliyeibiwa arudishiwe mali yake. Kutumia mali ya wizi ni
dhuluma, ni wizi.
Uwoya alikamatwa na simu ya wizi aina ya iPhone 5,
kwa hiyo kama aliuziwa, na kwa mujibu wa tafsiri ambayo nimeielezea hapo
juu ni wazi kwamba yeye siyo raia mwema. Ukweli uzidi kusimama kwamba
hafai kuitwa kioo cha jamii.
Je, ni tamaa ya kutaka vitu vizuri
wakati pesa hana? Ajioneshe mjini kwamba anamiliki iPhone 5 kumbe ni ya
wizi, ameipata kimagumashi. Namshauri Uwoya aache mtindo wa kuishi
kimagumashi, kama hana akubali hali halisi. Si kulazimisha maisha ya
gharama, matokeo yake ndiyo haya.
ANGEMTII MUMEWE YASINGEMFIKA HAYA
Nikiongoza jopo la waandishi kutoka Global Publishers Ltd, mwaka jana, tulifanikisha kumsuluhisha Uwoya na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutokana na mgogoro wa nguvu ambao ulikuwa unaitikisa ndoa yao.
ANGEMTII MUMEWE YASINGEMFIKA HAYA
Nikiongoza jopo la waandishi kutoka Global Publishers Ltd, mwaka jana, tulifanikisha kumsuluhisha Uwoya na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutokana na mgogoro wa nguvu ambao ulikuwa unaitikisa ndoa yao.
Malalamiko
ya Kataut yalijikita katika uaminifu, kwamba Uwoya alikuwa anaonesha
alama nyingi kuwa si mwaminifu kwenye ndoa yao. Mume huyo, alisema
kwamba amenunua vifaa na kuanzisha kampuni ili mkewe ajisimamie katika
kazi zake za filamu lakini mke hataki.
“Analipwa pesa kidogo ambayo
akifanya shopping tu zinakwisha, maprodyuza wanapata fedha nyingi, yeye
anafanya kazi, anauza sura tu lakini pesa hakuna. Nataka atengeneze
filamu zake ili apate pesa za kuonekana lakini haelewi wakati kila kitu
nimeshanunua,” Kataut alilalamika.
Kataut alikuwa na nia ya dhati
kabisa ya kumwokoa Uwoya na pengine kama angefuata mwongozo wa mumewe
leo hii asingeporomoka kama alivyo. Pengine yanayomkuta leo ni malipo ya
kile ambacho alimtendea mwanamme huyo.
Mke wa mtu kunaswa hotelini
na kijana wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ni aibu sana! Kabla ya
hapo zilishaibuka stori kwamba amegombana na supastaa Jacqueline Wolper
kisa mwanaume. Alimtesa sana Kataut wa watu.
Akiwa yupo ndani ya
ndoa, akaingia kwenye mgogoro na boyfriend wake wa zamani, Hamis
Ramadhan Baba ‘H-Baba’, akadai eti katika wanaume wake wote waliopita,
ambaye hawezi kurudiana naye ni H-Baba. Huyu ni mke wa mtu.
Tafsiri;
kumbe pamoja na kuwa kwenye ndoa, anaweza kurudiana na wanaume wake wote
waliotangulia isipokuwa tu H-Baba. Je, unamuonaje huyo? Ni mke wa mtu
kweli?
Mke wa H-Baba, Flora Mvungi naye akamvaa Uwoya, akamchamba, wakachambana. Mke wa mtu anagombana na mwanamke mwingine kisa mwanaume tofauti na mumewe. Ninaposema hafai kwenye jamii namaanisha kweli.
Mke wa H-Baba, Flora Mvungi naye akamvaa Uwoya, akamchamba, wakachambana. Mke wa mtu anagombana na mwanamke mwingine kisa mwanaume tofauti na mumewe. Ninaposema hafai kwenye jamii namaanisha kweli.
Matukio
ambayo anakumbana nayo hususan hili la wizi wa simu, achukue kama
changamoto na ajisahihishe pale alipojikwaa. Amwangukie mumewe pengine
mambo yakamnyookea. Iwe kama ameiba yeye moja kwa moja au aliuziwa,
ajisahihishe.
CHANZO CHA HABRI NI GLP
No comments:
Post a Comment