Msanii
mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa
Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku wa kumakia
leo,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye
tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
Madansa
wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku
wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani
Mara,ambapo tamasha la fiesta 2013.
Anajiita
tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani
wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la fiesta 2013 likiendelea hivi
sasa ndani ya uwanja wa Karume.
Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
Kundi
la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la
serengeti fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Karume mjini
Musoma mkoani Mara.
Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man
akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji
wa Musoma.
Anaitwa
Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele
ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la fiesta usiku wa
kuamkia leo
Makamuzi yakiendelea jukwaani
Sehemu ya umati wa watu.
Msanii
wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga
hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku wa kuamkia leo wakati wa tamasha la
fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma
mkoani Mara.
Kundi
la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature
wakilishambulia vyema jukwaa usiku wa kuamkia leo kwa staili yao mapanga
shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
Mashabiki wa tamasha la fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume.
Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume .
Mwanadada
Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya
watazamaji waliojitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la fiesta
2013.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani
Watu
kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo
kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza.
Wakali
wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na
Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.
No comments:
Post a Comment