Mbeya.
Yanga imetamba kuwa inarudi Dar es Salaam kwenye kapeti na sasa mashabiki wake wasubiri raha tu na heshima wataanza kuirudisha mechi yao ijayo na Azam FC kwa sababu walizocheza Mbeya zilikuwa na changamoto nyingi kwao.
Yanga imetamba kuwa inarudi Dar es Salaam kwenye kapeti na sasa mashabiki wake wasubiri raha tu na heshima wataanza kuirudisha mechi yao ijayo na Azam FC kwa sababu walizocheza Mbeya zilikuwa na changamoto nyingi kwao.
Ingawa imekiri kuwa mechi yao na Prisons wachezaji wao walikosa umakini wakaruhusu bao la kusawazisha.
Yanga itacheza na Azam FC Jumapili baada ya
kumaliza mechi zao za Mbeya walizotoka sare ya 1-1 na Mbeya City na sare
ya 1-1 na Prisons ya Mbeya.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro aliliambia gazeti hili kuwa, baada ya wakati mgumu waliokutana nao katika mechi hizo sasa wanarudi kwao.
“Tunarudi nyumbani kwenye kapeti sasa, heshima itarudi tu kuanzia mechi yetu na Azam,” alisema Minziro.
“Azam ni timu ngumu lakini imani yangu tutashinda. Unajua mechi za mkoani zina changamoto nyingi sana kama ulivyoona mwenyewe,” alisema Minziro ambaye pamoja na mkuu wake, Ernest Brandts walilalamikia ubovu wa uwanja na hali ya hewa.
Akizungumzia sare na Prisons, Minziro alisema:
“Tatizo lilikuwa kwenye umakini, wachezaji kwa nafasi zote hawakuwa
makini, ndivyo ilivyokuwa.”
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 6, watani wao wa jadi, Simba wanaongoza
ligi kwa pointi 10, wanafuatiwa na Ruvu Shooting na JKT Ruvu ni ya tatu.
No comments:
Post a Comment