Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hakuna mjumbe wa Tume hiyo aliyetishia kujiuzulu licha ya kwamba wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hakuna mjumbe wa Tume hiyo aliyetishia kujiuzulu licha ya kwamba wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.
Amesema katika awamu ya pili ya kukusanya maoni kupitia Mabaraza ya Wilaya ya Katiba wajumbe hao wamefanya kazi ngumu huku wakikabiliwa na changamoto nyingi, lakini wamevumilia kwa sababu wanafuata sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema: “Naona kwamba wajumbe wa Tume wanaeleweka vibaya kwamba wanataka kujiuzulu, lakini jambo hilo halipo kwani wanafanya kazi kwa kufuata sheria.
“Ninachokifahamu ni kwamba kwenye mazungumzo yetu
ya kawaida na kutoa mawazo tofauti, wajumbe walieleza kuwa kipindi hiki
cha kukusanya maoni kwenye Mabaraza ya Katiba wamefanya kazi kwenye
mazingira magumu na kulalamikiwa, wengine kwa sababu ya changamoto
walisema kuna haja gani ya kuendelea si tutoke tu, lakini haikuwa na
maana ya kujitoa.”CHANZO CHA HABARI NI GAZETI LA MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment