Young
Africans Siku ya jana imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Ruvu
Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika dimba la
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho ilipoteza kwa
kufungwa na Azam FC mabao 3-2 iliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha
inapata ushindi katika mchezo huo na ndivyo ilivyokua.
Ikiwatumia
washambuliaji wake Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na
Mrisho Ngassa, Young Africans ilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa
timu ya Ruvu Shooting lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake
kuliiinyima bao la mapema.
Dakika ya 27, Saimon Msuva alipoteza
nafasi ya wazi ya kufunga akiwa yeye na mlinda mlango Abdu Juma Seif
huku Hamis Kiiza pia akishindwa kutumia nafasi kama hiyo dakika ya 33 ya
mchezo.
Washambuliaji wa Ruvu Shooting walifanya mashambulizi
langoni mwa goli la Yanga kupitia kwa Cosmas Lewis, Jerome Lembele na
Elias Maguli lakini umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa kikwazo kwao
kuweza kuziona nyavu za Ally Mustapha 'Barthez'.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 1-0 Ruvu Shooting.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Athuman
Idd 'Chuji aliyechukua nafasi ya Frank Domayo mabadiliko yaliyopeleka
watoto wa Jangwani kuutawala mchezo katika sehemu ya kiungo.
Dakika
ya 63 mshambuliaji Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao la kwanza na la
ushindi baada ya kuitumia vizuri krosi ya Mrisho Ngassa aliyemtoka
mlinzi Stephano Mwasika na kupiga krosi iliyomkuta mfugaji aliyefunga
bao hilo maridadi na la msimu.
Mara baada ya bao hilo Yanga
iliendelea kufanya mashambulizi langoni mwa Ruvu Shooting lakini mpira
uliopigwa na Didier Kavumbagu uliokolewa na golikipa Abdul Juma Seif na
kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1- 0 Ruvu Shooting.
Mara
baada ya mchezo kocha mkuu Ernie Brandts amesema anashukuru vijana wake
wamepigana kuhakikisha wanapata ushindi katiika mchezo wa jana, ukizingatia
timu ilikua imetoka kupoteza mchezo wake wa mwisho.
Ushindi huu
wana Yanga wote, tunaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo
unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumamosi ijayo.
Young Africans: Mustapha, Twite, Luhende, Yondani, Nadir, Domayo/Chuji, Msuva.Nizar, Niyonzima, Kavumbagu, Kiiza, Ngassa
No comments:
Post a Comment