Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama
mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa
sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.
Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine,
haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho
kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya
show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni
mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.
Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama
za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene
amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya
kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na
amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha
siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka
kwa milioni 35.
Show yake ya TV imeshaanza kuonekana Tanzania pamoja
na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii kubwa ya
kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba zao
zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.
Show kama hii ambae inaitwa Extreme Makeover: Home Edition inapatikana kwenye BBC Lifestyle ikiletwa kwako kila siku saa 18:10 CAT.
Show kama hii ambae inaitwa Extreme Makeover: Home Edition inapatikana kwenye BBC Lifestyle ikiletwa kwako kila siku saa 18:10 CAT.
No comments:
Post a Comment