Wanasoka wa zamani John Barnes na Lucas
Radebe wamesema siri kubwa ya mafanikio yao katika mchezo wa soka
ilikuwa ni kutoweka mbele masilahi binafsi kama ilivyo kwa vijana wa
sasa, wameyasema maneno hayo siku ya jana kwenye kongamano la SOCCEREX
linalofanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban.
Beki wa zamani wa vilabu vya Kaizer
Chiefs,Leeds Utd ya England pamoja na kikosi cha Bafana Bafana Lucas
Radebe amesema wakati anachipkia kwenye mitaa ya Soweto yeye na vijana
wenzake walikuwa wakiugombania mpira mmoja uliokuwa unamilikiwa na
kijana mwenzao mtaani kwao, '' hatukuwa tunacheza ili tupate pesa pamoja
na umaskini mkubwa uliokuwa unatukabili,bali mapenzi tuliyokuwa nayo
juu ya mchezo wa soka ndio yalitusukuma sana kuucheza mchezo huo ''.
Naye kiungo wa zamani wa kimataifa wa
England na vilabu vya Watford na Liverpool John Barnes amesema
kinachowasukuma vijana wengi siku hizi kucheza soka ni ndoto zao za
kuvichezea vilabu vikubwa ulimwenguni kama vile FC BARCELONA na CHELSE,
'' siku hizi vijana wengi wanacheza ili wasajiliwe na vilabu
vikubwa,ikitokea hajasajiliwa basi wanaanua kuachana na mchezo wa
soka''.
No comments:
Post a Comment