NYUMBA ya Mchungaji Paul Ndalama (70) wa kanisa la Anglikana imeungua moto maeneo ya Moshi wilaya ya Ilala.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala Marietha Minagi alisema tukio hilo
limetokea juzi saa 12:45 katika mtaa wa Moshi katika kanisa la
Anglikana.
Minagi alisema moto ulizuka ghafla kwenye nyumba yenye vyumba vitatu
vya kulala, jiko, choo na bafu na kuteketeza nyumba yote pamoja na mali
yote iliyokuwemo ndani.
Minagi alisema nyumba hiyo inamilikiwa na kanisa la Anglikana. Mwenye
nyumba hakuwepo wakati wa tukio. Chanzo cha moto hakijafahamika.
Katika tukio jingine, mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na
umri kati ya miaka 30-35 amefariki baada ya kugongwa na gari maeneo ya
Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Camillius Wambura alisema tukio
hilo limetokea juzi majira ya saa nane usiku katika barabara ya Kawawa
eneo la Magomeni Mikumi.
Wambura alisema mwanaume huyo aligongwa wakati anavuka barabara
kutoka kushoto kwenda kulia na gari ambalo dereva wake hajulikani
aliyekuwa anatokea Magomeni kuelekea Kigogo; marehemu alikufa papo
hapo.
Maiti imehifadhiwa hospitali ya Muhimbili na msako wa kumtafuta dereva aliyekimbia baada ya ajali kutokea unaendelea.
No comments:
Post a Comment