MSHAMBULIAJI Fernando Torres anatumai kurejea uwanjani baada ya wiki tatu, kufuatia kuumia goti juzi nchini Romania.
Torres alitolewa nje dakika za mwanzoni
katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Chelsea ikishinda 4-0 dhidi ya Steaua
Bucharest Jumanne, lakini vipimo vimethibitisha hana maumiu makubwa.
Arakosa safari ya Norwich Jumapili,
ambayo tayari asingecheza kwa sababu ya kutumikia adhabu kutokana na di
nyekundu aliyopewa dhidi ya Tottenham.
Anatarajiwa kurudi kuichezea Hispania
katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Belarus na Georgia,
lakini Chelsea wanatumai kuwa naye tena mshambuliaji wao huyo kabla ya
mwishoni mwa mwezi.
Mdogo mdogo: Torres akitoka nje dakika ya 11 juzi kumpisha Samuel Eto'o baada ya kuumia
No comments:
Post a Comment