Baadhi ya wachezaji wa Yanga SC.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
inakamilisha raundi ya kumi na moja leo (Oktoba 29 mwaka huu) kwa mechi
tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa
mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu
zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati
ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati
Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu
kwenye uwanja huo huo.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal
Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT
(Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es
Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo
Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa
Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani
United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs
Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Chanzo ni GLP.
No comments:
Post a Comment