MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne
iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka
kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina
ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini,
alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda
mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio
wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya
Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema
shuhuda huyo.
Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari
hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas
Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo
hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru.
Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari
walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka
naye chini.
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo
la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu
mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.
Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa
Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe
Mlimani City.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba
mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila
nawafahamu,” alisema Mbaga.
Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment