MWIGIZAJI na mwanamuziki mwenye mbwembwe nchini Hemed PHD
ametoa onyo kwa wanawake ‘wanaomsarandia’ wakitaka penzi lake wamwache
atafute maisha kwani huu ndio wakati wake.
Hemed PHD.
Amesema kitendo cha baadhi ya wanawake kuacha
shughuli zao na kuanza kumfuatilia wakitaka awe mpenzi wao kimekuwa
kikimkera sana hasa ikizingatiwa kuwa hakiendi sawa na utamaduni kwani
mwanamume ndiye anayetakiwa kumfuata mwanamke.“Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwangu kukaa na namba moja ya simu kwani nikishaona nasumbuliwa sana huwa nalazimika kubadilisha ili kuepusha usumbufu,” anasema.
Anaongeza kuwa huwa anawatosa wanawake wanaomfuatilia kwa kuwa anaamini hawamtakii mema : “Ninahisi wengine wanataka kuniharibia tu, huwezi jua labda ni mbinu tu za kutaka kunipoteza kwenye ramani.”
Hemed anasema kipaumbele chake sasa ni kazi na ndiyo maana muda mwingi amekuwa haonekani au kusikika.
“Nimekuwa bize katika uigizaji kwani mara nyingi nakuwa sehemu nikifanya kazi , ninaamini katika kazi na ndio sababu nimekuwa nikijituma kwa kadri ya uwezo wangu,” anasema. Akieleza kuhusu familia yake Hemed anasema kimsingi yupo singo na hana mpango wa kuoa kwa sasa, ispokuwa anachofanya ni kumhudumia mama yake pamoja na ndugu wengine wa familia yake jambo ambalo ni la kawaida kabisa kwa kijana yeyote mwenye umri wake.
“Watu wengi hudhani kwamba kutokana na makeke niliyokuwa nayo labda naweza kuwa kwenye mipango ya kuvuta jiko kwa sasa lakini ukweli ni kwamba sina mpango huo,” anasisitiza.
“Kuhusu uhusiano siwezi kukataa kuwa nilikuwa na mpenzi lakini nimeachana naye miezi minne iliyopita baada ya kutokea kutofautiana kati yetu,” anasema.
Anasema kwa sasa anaangalia mbele akiwekeza nguvu zake katika kutafuta pesa zaidi.
Hemed ambaye pia aliwahi kujizolea umaarufu katika mashindano ya Tusker Project Fame akiwa kama mshiriki, anasema amekuwa na mapenzi ya kweli katika kazi zake na mara nyingi amekuwa haoni shida kuzitendea haki.
“Kwangu filamu ama muziki ni kazi, hivyo huwa sina mzaha kabisa wakati ninapokuwa naigiza au nafanya muziki. Mara nyingi akili yangu huwa ni katika kuhakikisha ujumbe uliokusudiwa unawafikia walaji wangu,” anasema
Hadi sasa katika kazi ya uigizaji anasema tayari ameigiza filamu zaidi ya 30.
“Najua watu wengine walioko nyuma ya kamera walifanya kazi kubwa sana lakini binafsi siachi kujipongeza ninapoangalia filamu hizo kwani nimejaribu kuonyesha uwezo wangu halisi,” anafafanua.
Anasema kimsingi kazi ya uigizaji inahitaji umakini na umahiri mkubwa kwani wakati mwingine kitendo cha kuzembea katika kazi moja kinaweza kukusababishia ukaharibu kazi nyingine . Akizungumzia kuhusu muziki, Hemed anasema muziki ni sehemu ya kazi yake kama ilivyo kwenye filamu na katika kudhihirisha hilo mara kwa mara amekuwa akija na vitu vipya.Kwa sasa anatamba na singo yake ya Rest of My Life aliomshirikisha Mr. Blue.
“Naamini kila filamu ninayoigiza ni nzuri, lakini filamu ambazo
nazikubali zaidi ni pamoja na Red Cross ambayo niliigiza kama mchimba
madini wa Mererani na ‘For my Child,” anasema. Anasema mara nyingi
anapoangalia kazi hizo huwa anajisikia furaha sana.
“Najua watu wengine walioko nyuma ya kamera walifanya kazi kubwa sana lakini binafsi siachi kujipongeza ninapoangalia filamu hizo kwani nimejaribu kuonyesha uwezo wangu halisi,” anafafanua.
Anasema kimsingi kazi ya uigizaji inahitaji umakini na umahiri mkubwa kwani wakati mwingine kitendo cha kuzembea katika kazi moja kinaweza kukusababishia ukaharibu kazi nyingine . Akizungumzia kuhusu muziki, Hemed anasema muziki ni sehemu ya kazi yake kama ilivyo kwenye filamu na katika kudhihirisha hilo mara kwa mara amekuwa akija na vitu vipya.Kwa sasa anatamba na singo yake ya Rest of My Life aliomshirikisha Mr. Blue.
VIA MWANASPORTS.
No comments:
Post a Comment