Mwigizaji, muongozaji wa filamu na mmiliki wa kampuni wa filamu
ya 5effects William Mtitu amepata bahati ya kuongeza idadi ya
wanafamilia wake baada ya mke wake Jovitha Mtitu kujifungua salama mtoto
wao wa kwanza kwenye hospitali ya Regency jijini Dar es salaam hivi
majuzi.
Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja wa kijamii Mtitu aliandika…
“Nawashukuru madaktari wa hospital ya regency na kwa Dr mvungi
wakiongozwa na Dr getu kwa kusaidia mpaka mke wangu kujifungua salama na
sasa naitwa baba na mke wangu mama ,kwa kweli mungu awabaliki sana…”
Hali ya Mama na mtoto ni njema na wanaendelea vizuri. Hongera sana Mtitu na familia yako.
No comments:
Post a Comment