Kiungo wa Al Markhiya, Mwinyi Kazimoto.
Na Saleh Ally, NairobiKIUNGO wa Al Markhiya, Mwinyi Kazimoto, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Qatar, ameiongoza kushika nafasi ya tano kati ya timu 18.Akizungumza kutoka Qatar, Kazimoto amesema timu yake hiyo imeshika nafasi ya tano.
“Kwa sasa ligi imesimama na timu yao ya taifa imeingia kambini, lakini tupo katika nafasi ya tano,” alisema.
“Mwendo wetu si mbaya sana kutokana na ugumu wa ligi yenyewe lakini nina imani tutafanya vizuri.”
Kazimoto ndiye amekuwa kiungo tegemeo katika kikosi hicho, hasa katika uchezeshaji.
Pamoja na kuwa na upinzani mkubwa wa namba, Kazimoto amefanikiwa kumshawishi kocha wa timu hiyo kutokana na kiwango chake na sasa anampanga kila mechi.
HABARI NA GPL
No comments:
Post a Comment