Ndugu
 Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule 
ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani 
Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni 
 mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata 
na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
 Pichani
 chini, Ndugu Kinana akiwa amebeba tofali ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa
 ujenzi wa madarasa katika  shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika 
Halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha 
Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani 
Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na 
kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazi pia 
kuwa kama chama Imara lazima kihoji serikali juu ya  pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu
 Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani 
ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za 
Wanachi.
  Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha 
Katende  ndani ya halmshauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani 
Mbeya,ambapo Nape aliwatahadharisha wakaji wa mji huo kuwa makini na 
vyama vinavyojita vya siasa,kutokana na kuanza kupoteza dira na 
muelekeo.
 Katibu
 wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao 
akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwa ajili ya
 ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya 
Mwakaleli.
 Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na 
wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na 
kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
 Katibu
 wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa 
ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina 
mama wa Katende,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
 Mzee 
Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na 
pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero 
zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
Mbunge
 wa Wanawake Mkoa wa Mbeya  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi 
Katende.katika halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
 
 
 
 
 
 
 












 
No comments:
Post a Comment