EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, November 12, 2013

MLINZI WA DK MVUNGI AHUSISHWA SHAMBULIO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akionesha mapanga yanayodaiwa kutumiwa kumjeruhi Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi nyumbani kwake hivi karibuni. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima Dar es Salaam jana. (Picha na Mroki Mroki).

WATU tisa wanashikiliwa na Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma za kuvamia nyumbani na kumjeruhi Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mwanasheria mkongwe, Dk Sengondo Mvungi.
 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emannuel Nchimbi alisema jana Dar es Salaam kuwa baadhi ya watuhumiwa hao walikutwa na simu iliyoporwa nyumbani kwa Dk Mvungi pamoja na mapanga yanayodaiwa kutumika katika shambulizi hilo.
 

Dk Mvungi alivamiwa na kushambuliwa wiki iliyopita nyumbani kwake Kibamba na kupoteza fahamu kukimbizwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kabla ya kuhamishiwa Muhimbili ambako alilazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kishsa kupelekwa Milpark, Afrika Kusini ambako anatibiwa.

Waziri Nchimbi alisema baada ya mahojiano ya kina washukiwa hao walikiri kushiriki tukio hilo na walitoa ushirikiano wa kutosha hadi kupatikana kwa mapanga hayo na kigoda.
 

“Uchunguzi wa Polisi katika tukio hili umekamilika kwa asilimia 80, tumebakiza watu wachache walioshiriki na tunawahakikishia wananchi kuwa tutawakamata hivi karibuni,” alisema Nchimbi ambaye alifuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima na Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
 

Kova alitaja waliokamatwa kuwa ni Msigwa Mpopera ambaye ni mlinzi nyumbani kwa Dk Mvungi ambaye kwa mujibu wa Kova ndiye alikuwa kiongozi wa tukio hilo na kwamba aliongoza wenzake kufanya shambulio hilo.
 

Mwingine ni Chibango Magozi ambaye alikamatwa akiwa na simu iliyoibwa nyumbani kwa Dk Mvungi. Kamanda Kova alisema baada ya watuhumiwa hao kubanwa walitaja wenzao na kukubali kwenda kuonesha mapanga waliyotumia kutenda uhalifu huo.
 

Wengine wanaoshikiliwa ni Ahmed Ali, Zakaria Msesa, Manda Saluwa, Paul Jailos na Juma Khamis ambao wote ni wakazi wa Vingunguti; Longishu Semariki mwuza tumbaku (ugoro) katika eneo la Msimbazi na Msunga Makenza dereva wa bodaboda Kitunda.
 

“Upelelezi wa tukio hili umefanywa kwa kiwango cha juu na tunashukuru ushirikiano uliooneshwa na familia na vyombo vya habari,” alisema Kamanda Kova.
 

Alisema kazi iliyobaki sasa ni kukamilisha upelelezi na kupeleka jalada kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili atoe kibali cha kesi hiyo kwenda mahakamani.
 

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Kova alisema uhalifu aliofanyiwa Dk Mvungi hauhusiani na siasa kwani ushahidi unaonesha kuwa watuhumiwa walikuwa wanatafuta kipato.
 

Ulimboka, Kibanda
 

Alipoulizwa sababu ya upelelezi wa tukio la Dk Mvungi kuharakishwa, wakati kuna matukio kama ya Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka hadi leo Polisi iko kimya, Kova alisema watuhumiwa wa Dk Mvungi walipatikana haraka kutokana na ushirikiano wa vyombo vya habari na familia.
 

“Unajua katika tukio hili hazikuwapo habari za Polisi kuhusika au mhusika ni nani, haya mambo ya upelelezi ukishamtuhumu polisi wakati ndiye anafanya upelelezi wakati mwingine inakatisha tamaa,” alisema Kova.
 

Dk Nchimbi alifafanua kuwa matukio ya Dk Ulimboka na Kibanda yanaendelea kufanyiwa uchunguzi.
 

“Katika nchi zinazoendelea, upelelezi wa matukio mengine unafanyika hata miaka mitatu au minne na baadaye watuhumiwa wanakamatwa kirahisi.”
Wakati huo huo, Dk Nchimbi alisema katika kupambana na uhalifu nchini, Polisi itasambaza maofisa wake wapatao 200 kila tarafa ambao watashirikiana na Polisi Jamii kupambana na uhalifu.


CHANZO NI HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate