BAADA ya kukaa nje ya ulingo wa filamu kutokana na kukumbwa
na matatizo mbalimbali ikiwamo kumpoteza mumewe, mwigizaji wa filamu
nchini, Wastara Juma, anatarajia kupeleka sokoni filamu mpya
itakayojulikana kama Shaymah.
Akizumgumza jana jijini Dar es Salaam, Wastara
alisema filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni iitwayo Wastara Juma na
amewashirikisha waigizaji wenzie akiwamo Yusuph Mlela, Saumu Jabu
‘Nisha’ na wengineo.
Wastara alisema anatarajia kuisambaza filamu hiyo mwezi huu na
kuielezea kuwa imenena kisa cha kweli cha mapenzi yenye mafunzo ndani
yake na kudai kuwa kinaweza kumtokea mtu yeyote.
“Kwa muda mrefu sasa, nilikuwa nje ya sanaa kutokana na matatizo
ambayo wote mnayajua, lakini namshukuru Mungu kanipa roho ya ujasiri,
nakuja na ‘movie’ yangu mpya inayoitwa ‘Shaymaa’ ambayo imebeba
uhalisia wa kisa cha kweli,” alisema.
Wastara alisema kuwa filamu hiyo itatoa funzo kutokana na kisa
kilichobebwa, ambacho kinaweza kumkuta mtu yeyote ambaye atampoteza mtu
muhimu katika maisha yake na kumsababisha kuwa katika hali tofauti.
No comments:
Post a Comment