
Sudi
 Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu 
nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda 
kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa 
kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD 
alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho 
lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi 
kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na 
African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema 
peponi - ameen!
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment