



Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa
Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jana
Jumatano ameungana na Mabalozi wengine wanaoziwakilishi Nchi zao katika
Umoja wa Mataifa, kutia saini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa
katika Uwakilishi wa Kudumu wa Udachi ( Netherlandes) katika Umoja wa
Mataifa kuwakumbuka watu 298 waliopoteza maisha baada ya ndege
waliyokuwa wakisafiria ya MH17 inayomilikiwa la Shirika la Ndege la
Malaysia kuangushwa katika eneo la Mashariki ya Ukraine wiki iliyopita.
Idadi kubwa ya abiria hao walikuwa ni raia wa Udachi.
No comments:
Post a Comment