RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA AKIWA NA MAKAMU WAKE, GEOFREY NYANGE 'KABURU'. |
Uongozi wa Klabu ya Simba
umelivaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kauli yao ya kuzitaka klabu
kutojihusisha na wakili wa kujitegemea Damas Ndumbaro kupitia kampuni yake ya
Maleta & Ndumbaro Advocate.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa kwa
upande wao bado wanaendelea kumsapoti Ndumbaro kwa asilimia 100 kwa sababu wao
ndiyo waliomtuma na kudai kuwa watashirikiana naye kama kawaida katika masuala
ya soka.
“Kamati iliyoshughulikia suala hilo ni huru na
kwa upande wetu Simba tupo mstari wa mbele kuhusu suala hilo na tunamsapoti.
“Tutaendelea kumtumia Ndumbaro kama kawaida
kwani tunatetea haki yetu na tunapinga vikali makato ya asilimia tano ya
mapato.
“Hakuna waraka wowote tuliopewa klabu kuhusu
jambo hilo,” alisema Aveva.
TFF ilitangaza kumfungia Ndumbaro kujihusisha
na soka kwa miaka saba kutokana na kile kilichoelezwa kukiuka kanuni kadhaa za
shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment