WAKATI tukiwa
tunakaribia kumaliza mwaka 2014, msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’,
amedai kuwa hakuna jambo ambalo mastaa wa Bongo wamelifanya zaidi ya
kuchuma dhambi na kutumia muda mwingi kupigana majungu kuliko kumcha
Mungu kwa matendo mema.
Msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na gazeti hili, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya
filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo
ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi
kuchafuana kwa kupigana majungu.“Ni kweli mwaka umeisha lakini lazima tujue wapi tumekosea, lakini wasanii wetu hawana roho ya kuamini kuwa Mungu yupo ndiyo maana wanapigana majungu kila kukicha.
Tangu kifo cha kipenzi Kanumba kutokea nilisemwa sana na baadhi ya wasanii wakidai kuwa siwezi kuwika tena lakini wanasahau kuwa niko bize na kazi ya Mungu na si kupiga majungu au kukaa kijiweni kumsema mtu,” alisema Mainda.
No comments:
Post a Comment