MAGWIJI wa nyimbo za
taarabu nchini, Mfalme Mzee Yussuf na Malkia Khadija Omar Kopa
wameungana pamoja kuimba wimbo wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na
kufanya onyesho kubwa la uzinduzi wa video yake mwishoni mwa wiki katika
onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar
es Salaam.
Onyesho hilo lililohudhuriwa na mashabiki
lukuki lilisindikizwa na bendi zinazoongozwa na wakali hao, Jahazi
Modern Taarab na TOT ambazo nazo zilitoa burudani ya kutosha kwa kupiga
nyimbo zao mbalimbali.
Magwiji wa nyimbo za taarabu nchini, Mfalme Mzee Yussuf na Malkia Khadija Omar Kopa wakiimba kwa pamoja.
Wimbo huo wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake umeandaliwa maalum kwa
ajili ya kampeni ya Tunaweza ambayo inasimamiwa na mashirika ya
Kivulini, WLAC, Tree of Hope, WOWAP, CORDS na Oxfam.
No comments:
Post a Comment