Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sikonge mkoani
Tabora wakati alipopita kukagua barabara za mkoa huo. Dkt. Magufuli
aliwaahidi wananchi hao wa Sikonge kuwa Serikali itaanza ujenzi wa
barabara ya Mpanda-Tabora kupitia Sikonge yenye zaidi ya kilomita 359
itakayofadhili na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Sikonge mara baada ya kuwahutubia.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila kushoto akizungumza na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli kabla ya kuhutubia mkutano kwa wananchi wa
Tabora. Waziri Magufuli aliwaeleza wananchi kuwa Wizara ya Ujenzi
itawasimamia kikamilifu Wakandarasi wanaojenga barabara katika mkoa huo
na kuhakikisha miradi yote inakwisha kwa wakati.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Tabora kuhusu ujenzi barabara za mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisalimiana na wananchi mara baada ya mkutano wake alioufanya Tabora mjini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila akihutubia wananchi katika mkutano huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mlele Col.Ngemela Eslom Lubinga akimuonesha Waziri wa
Ujenzi ramani ya Wilaya ya Mlele katika sehemu linapojengwa daraja la
Kavuu lenye urefu wa mita 84 litakalounganisha Kijiji cha Kibaoni na
makao makuu ya Wilaya hiyo Inyonga.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Inyonga Wilayani Mlele ambapo barabara ya Mpanda-Tabora itapita.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele
Col.Ngemela Eslom Lubinga mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya Mkuu
huyo wa wilaya inayojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Wilayani Mlele
mkoani Katavi.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Tabora mara baada
ya kukugua mradi wa barabara ya Sikonge-Tabora.Picha zote na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment