Waliokaa
kutoka kushoto ni Ibrahim Masoud 'MAESTRO' na Maulid Kitenge.
Waliosimama kutoka kushoto ni Oscar Oscar, Senkondo Rashidi, Mussa
Kawambwa, Sudi Mkumba, Yusuph Mkulena Francis Mhando.
Sports Headquarters (Makao makuu ya michezo) ni kipindi kipya ndani
ya E FM kilichoanza mnamo tarehe 2/Feb/2015. Kipindi hichi kinachoruka
kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kitakuwa kinaruka hewani kuanzia saa
tatu asubuhi mpaka saa sita mchana.Watangazaji wa kipindi hiki ni Maulid Kitenge, Ibrahim Masoud “Maestro”, Mussa Kawambwa, Oscar Oscar na Yusuph Mkule huku waandaaji wakiwa ni Senkondo Rashidi, Francis Mhando na Miraji Mwako.
Radio nyingi nchini Tanzania zimekuwa na vipindi vinavyofanana kuanzia majira ya saa tatu asubuhi mpaka saa saba mchana (vingi vikiwa vinawalenga wanawake) ila kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na makampuni mbalimbali imesadikika kuwa vipindi vinavyopendwa ni Michezo, Dini na habari.
Katika radio zote nchini vipindi vya michezo vinakuwa kuanzia majira ya saa moja usiku mpaka saa nne usiku.
EFM imeamua kufanya mageuzi kwa kuleta masaa matatu ya michezo katika muda ambao wengi hawakuwahi kufikiria na kwa muda mfupi tu, toka kipindi kilipoanza kuruka hewani teyari mapokeo ni makubwa sana na wadau wameanza kuomba muda uongezwe!
Sports Headquarters na E-SPORTS ni Vipindi ambavyo vitakuwa vinashirikiana kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment