Mzee Yussuf anaweza kuwa mfano mzuri sana kwa wanamuziki wengine kwa
namna anavyowekeza ili asitetereke pale atakapoamua kuupa mkono wa kwaheri
muziki au muziki kumpa mkono wa kwaheri.
Mfalme huyo wa taarab anayemiliki kundi la Jahazi Modern Taarab, ana
mradi mkubwa wa kuuza vifaa vya ujenzi ikiwemo cement na mtofali ya kisasa huko
Chanika na Kigamboni.
Jengo lenye maduka likiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi
Hapa kutakuwa na maduka ya vifaa vya ujenzi na magari
Uwanja wa Mzee Yussuf unavyoonekana kwa mbele
Mzee Yussuf ana viwanja viwili vyenye mradi wa kufyatua matofali huko Chanika
na kimoja kingine Kigamboni. Ni miradi mikubwa ambayo iko chini ya mwamvuli wa
kampuni yake inayojulikana kama M.Y. Contractors.
Katika kurahisisha kazi za M.Y. Contractors, Mzee Yussuf anamikili
malori ya Scania na Fuso ambayo hutumika kubeba michanga, matofali na vifaa
vingine kwaajili ya viwanda vyake pamoja na wateja wake.
Hakika Mzee Yussuf yuko vizuri sana kwani Saluti5 ilipotembelea moja
ya viwanja vyake vya Chanika, ikashuhudia ujenzi wa mjengo wa maana utakaokuwa
na gorofa moja kwaajili ya makazi yake na familia yake.
Lakini ndani ya uwanja huo mkubwa unaoweza kujenga hata nyumba 20 za
kawaida, kuna nyumba nyingine ya maana ambayo nayo ujenzi wake haujakamilika.
Ni nyumba mbili za maana kwa mpigo.
Katika kuonyesha kuwa kiwanja hicho ni kikubwa kupindukia, sehemu ya
mbele Mzee Yussuf amejenga jengo lenye maduka manne ambayo yote yatahusiana na
kazi za M.Y. Contractors lakini pia nyuma ya maduka hayo kuna vyumba vingine
ambavyo vitatumika kama ofisi yake na maafisa wengine wa kampuni.
Mzee Yussuf ameidokeza Saluti5 kuwa ameanzisha pia mradi mkubwa wa
kufuga kuku wa nyama na mayai (wa kisasa na kienyeji) huko Kigamboni.
Kwa namna alivyowekeza Mzee Yussuf, hakuna ubishi kuwa nyota huyo sasa
anaweza kabisa kuishi bila kutegemea pato la muziki.
Mama muuza samaki ni akifanya biashara yake ndani ya uwanja wa Mzee Yussuf, ujirani uliotukuka!
Mzee Yussuf akimuunga mkono jirani yake
Mzee Yussuf akiangalia namna kazi zinavyoendelea
Sehemu ya mradi wa matofali inavyoonekana
Sehemu ya pili ya mradi wa matofali
Baadhi ya vitendea kazi
Hii ni nyumba mpya ya Mzee Yussuf inavyoonekana kwa nyuma
Nyumba mpya ya Mzee Yussuf inavyoonekana kwa ubavuni
Inavyoonekana kwa mbele
Sehemu ya mbele kwa karibu zaidi
Si mjengo wa kitoto!
Mzee Yussuf mbele ya mjengo wake
Hii ni nyumba nyingine ya Mzee Yussuf ambayo ipo kwenye uwanja wake huo huo wa Chanika
Huu nao ni mjengo wa haja
Jengo lenye maduka linavyoonekana kwa nyuma
Mzee Yussuf akifurahia upepe mwanana wa Chanika
No comments:
Post a Comment