BINTI wa marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown amefariki dunia jana baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani bafuni.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22, huku akivutiwa kuwa muigizaji na mwimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
Msemaji wa familia ya marehemu, Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake,”hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu, tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita”.

Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka bafuni Januari 31, mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amepoteza fahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.
Itakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi, Whitney Houston alikutwa pia bafuni akiwa amepoteza fahamu baada ya kuzidisha kiwango cha dawa za kulevya na pombe na baadaye kupoteza maisha.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown, magwiji wa muziki wa miondoko ya R&B.
No comments:
Post a Comment