Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.
Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.
Wakati
gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa
staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa
taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi
fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha
chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.
Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
CHANZO: GPL

No comments:
Post a Comment