Sweetbert Lukonge,
Dar es Salaam
SIKU chache baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, kutimkia zake nchini Denmark katika Klabu ya Sonderjyske Fodbold, amemvuta nchini humo nyota wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.
Okwi amejiunga na Sonderjyske Fodboldn hivi karibuni baada ya uongozi wa klabu hiyo kuvutiwa na kazi yake ambayo amekuwa akionyesha uwanjani akiwa na kikosi cha Simba na atakuwa akilipwa kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 20) kwa mwezi.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi.
Kutokana na hali hiyo, Okwi atakuwa ni mchezaji wa pili kutoka katika Klabu ya Simba kulipwa fedha nyingi nje ya nchi baada ya Mbwana Samatta wa TP Mazembe ambaye pia anachukua kitita cha dola 10,000 kwa mwezi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema mafanikio ya Okwi ni jambo ambalo kila mmoja angependa kulipata na hata yeye kama ikitokea atapata bahati kama hiyo aliyoipata Okwi, basi yupo tayari kuondoka Yanga na kwenda kucheza soka la kulipwa nchini humo kwa sababu hakuna mchezaji asiyependa mafanikio.
“Kwanza kabisa napenda kumpongeza Okwi kwa bahati hiyo aliyoipata kwani ni jambo zuri na ninamwombea kwa Mungu afanye vizuri.
“Bahati hiyo aliyoipata Okwi hata kama ningeipata mimi ni lazima ningeenda kwa sababu kila mchezaji anapenda mafanikio na siyo kitu kingine na kama itatotea na itakuwa na maslahi mazuri, nitaongea na viongozi wangu na wakiniruhusu nitaenda kufanya kazi,” alisema Tambwe.
Kutokana maneno hayo ya Tambwe, kwa namna moja au nyingine unaweza kusema kuwa Okwi amemvutia nyota huyo kwenda Denmark kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
No comments:
Post a Comment