Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HAYAWI hayawi, hatimaye yametimia, lile tamasha la burudani lililosubiriwa kwa hamu kubwa la Usiku wa Mastaa Temeke hatimaye litashuhudiwa leo na mashabiki wa muziki wa Kibongo, likitarajiwa kushushwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhiem jijini Dar es Salaam.
Dhamira kubwa katika tamasha hilo ni utoaji wa zawadi kwa mastaa balimbali hapa nchini ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kuiwakilisha vema Wilaya ya Temeke na viunga vyake.
Banana Zoro
Mratibu wa tamasha hilo, Richard Yalomba amesema mbali na kutoa zawadi hizo, pia siku hiyo kutatawaliwa na burudani za kutosha kutoka Kundi la FM Academia na Isha Mashauzi ambazo zitaanza saa moja usiku mpaka majogoo.
Happiness Millen Magesse
Miongoni mwa mastaa watakaoondoka na medali kutokana na mchango wao kuwa ni wanamitindo, Happiness Millen Magesse na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature, mkali wa Bongo Fleva, Banana Zorro na gwji kutoka Kundi la TMK Wanaume Family, Chegge.
Chege
Jokate
No comments:
Post a Comment