Mtu mmoja Silvester Prosper (44), amejinyonga kwa sababu ya kuambiwa analea watoto wawili wasio wakwake.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya
Kinondoni, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 mwaka
huu, majira ya saa 3:00 maeneo ya Kinondoni Gundula.
Kamanda Kenyela alisema hivyo Silvester alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani ambayo aliifunga chumbami kwake juu ya kenchi.
Hata hivyo, kamanda Kenyela alisema
kwamba marehemu aliacha ujumbe uliokuwa ukisema “nimechoshwa na maisha
ya Duniani, sistahili kuwepo hasa kwa mke wangu aitwaye Christina
Kilahilo (32) mkazi wa Kinondoni kwa kisa cha kuniambia watoto alionao
siyo wangu.”
No comments:
Post a Comment